Ciro
Immoble akishangilia baada ya kuifungia Italia mabao mawili dakika ya
nane na 33 katika ushindi wa 9-1 dhidi ya Armenia kwenye mchezo wa Kundi
J kufuzu Euro 2020 usiku wa jana Uwanja wa Renzo Barbera mjini Palermo.
Mabao mengine ya Italia yalifungwa na Nicolo Zaniolo dakika ya tisa na
64, Nicolo Barella dakika ya 29, Alessio Romagnoli dakika ya 72,
Jorginho kwa penalti dakika ya 75, Riccardo Orsolini dakika ya 77
na Federico Chiesa dakika ya 81, wakati bao pekee la Armenia limefungwa
na Edgar Babayan dakika ya 79. Kwa ushindi huo, Italia ambayo tayari
imekwishafuzu Euro ya mwakani, inafikisha pointi 30 katika mchezo wa 10,
sasa wakiizidi pointi 12 Finland inayofuatia katika nafasi ya pili
Home
»
»Unlabelled
» ITALIA YAFANYA BALAA ULAYA, YAISHINDILIA ARMENIA 9-1 KUFUZU EURO 2020
Wednesday, November 20, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment