Taarifa
zilizoenea zinaeleza kuwa baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems
kuondoka kuelekea kwao Ubelgiji, kuna uwezekano klabu hiyo ikaachana
naye.
Aussems
aliondoka nchini jana kuelekea kwao ikielezwa sababu ni matatizo ya
kifamilia lakini taarifa za ndani zinasema anaweza akafutwa kazi.
Inatajwa
kuwa kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika mapema dhidi ya UD Songo
katika hatua ya awali ndicho kinachomhukumu Aussems ndani ya Simba.
Mbali
na hilo, mwenendo wa kikosi hicho licha ya kuwa na matokeo mazuri
katika ligi, namna kikosi kinavyocheza hakiwafurahishi wadau wengi wa
Simba pamoja na mashabiki jambo ambalo linaelezwa linaweza sababisha
kibarua chake kuota mbawa.
Leo
hii kikosi hicho chini ya Msaidizi wake Denis Kitambi kitakuwa na
mchezo wa kirafiki majira ya saa mbili za usiku dhidi ya JKT Tanzania,
mechi ikichezwa Azam Complex.

0 comments:
Post a Comment