Jose
Mourinho amekuwa kocha wa pili duniani katika mchezo wa soka kulipwa
fedha nyingi zaidi baada ya kuanguka saini ndani ya klabu ya Tottenham
ambayo itakuwa inampatia kiasi cha pauni milioni 15 kwa mwaka.

Kusaini kwake tu, kwa miamba hiyo ya soka ya Kaskazini mwa jiji la London, Mourinho atakuwa anapokea kitita cha fedha mara mbili ya mshahara ambao alikuwa akilipwa kocha aliyetimuliwa kazi, Mauricio Pochettino.
Hii
ni kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu ya Tottenham, kumwajiri
kocha mwenye kariba ya Mourinho ambaye tayari ameshinda mataji 25 kwenye
taaluma hiyo huku wakitoa kitita kinono.

Mourinho
sasa atakuwa akipokea mshara wa Pauni Milioni 15 kwa mwaka kiasi
ambacho kinamfanya kushika nafasi ya pili (2), kwa malipo ambayo wanapa
makocha wanaofundisha mchezo wa soka.
Mreno
huyo anakuwa nyuma ya Pep Guardiola ambaye anashika nafasi ya kwanza
akipokea Pauni Milioni 20 baada ya kuongeza mkataba wake ndani ya
Manchester City msimu uliyopita 2018 ambao atashuhudiwa akiwa hapo kwa
miaka mingine miwili.
Mhispania huyo
ndiyo kinara kwa makocha wote wa soka duniani akipokea kiasi hicho cha
pesa pauni milioni 20 kwa mwaka na akidhihirisha uhalali wa yeye kupokea
mkwanja huo baada ya kuchukua ubingwa wa Premier League ‘back-to-back’.
0 comments:
Post a Comment