PATRICK
Aussems, kocha mkuu wa Simba ambaye kwa sasa yupo nchini Ubelgiji ametangaza
hali ya hatari kwa wapinzani wa Simba ambao atakutana nao kwenye mchezo wao
unaofuata wa ligi.
Aussems
aliondoka nchini Tanzania Juzi kimyakimya na kurejea nyumbani kwao Ubelgiji kwa
kile alichokieleza kuwa ni kutokana na sababu zake binafsi na ameahidi kurejea
leo akiwa na hasira za kupata pointi tatu za Ruvu Shooting iliyo nafasi ya nane
na ina pointi 15.
Kupitia ukurasa
wake wa Instagram Aussems amesema:” Niliondoka kwa sababu zangu binafsi
mwenyewe kwa siku mbili nitarejea kesho (leo) kwa ajili ya maandalizi  ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting
nazihitaji pointi tatu.
Championi
Jumatano lilizungumza na Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu ambaye alisema
kuwa hawezi kuzungumzia suala la kocha kwa kuwa bosi wao ameshazungumza.
“Bosi
amesema kuwa hajui alipo kocha sasa mimi nitazungumza nini hapo, zaidi ya
kufuata kile ambacho amesema CEO?  Mtendaji Mkuu) basi kwa kuwa mwajiri
hajui alipo mfanyakazi wake hakuna nitakachoweza kuzungumza,” alisema
Rweyemamu.
Simba
itashuka uwanja wa Uhuru Novemba 24 kumenyana na Ruvu Shooting mchezo wao wa 10
kwenye ligi ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 9 na imejikusanyia
pointi 22, imepoteza mchezo mmoja mbele ya Mwadui FC na imeshinda mechi saba na
sare moja mbele ya Tanzania Prisons.
0 comments:
Post a Comment