Patrick
 Aussems, kocha mkuu wa Simba ambaye kwa sasa yupo nchini Ubelgiji 
ametangaza hali ya hatari kwa wapinzani wa Simba ambao atakutana nao 
kwenye mchezo wao unaofuata wa ligi.
Aussems
 aliondoka nchini Tanzania Jumatatu ya wiki hii kimyakimya na kurejea 
nyumbani kwao Ubelgiji kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokana na sababu
 zake binafsi na aliahidi kurejea jana akiwa na hasira za kupata pointi 
tatu za Ruvu Shooting iliyo nafasi ya nane na ina pointi 15. Kupitia 
ukurasa wake wa Instagram Aussems amesema:”
"Niliondoka
 kwa sababu zangu binafsi mwenyewe kwa siku mbili nitarejea kesho 
(jana), kwa ajili ya maandalizi  ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting 
nazihitaji pointi tatu.
”
 Championi Jumatano, lilizungumza na Meneja wa  Simba, Patrick Rweyemamu
 ambaye alisema kuwa hawezi kuzungumzia suala la kocha kwa kuwa bosi wao
 ameshazungumza.
“Bosi
 amesema kuwa hajui alipo kocha sasa mimi nitazungumza nini hapo, zaidi 
ya kufuata kile ambacho amesema CEO? (Mkurugenzi Mtendaji) basi kwa kuwa
 mwajiri hajui alipo mfanyakazi wake hakuna nitakachoweza kuzungumza,” 
alisema Rweyemamu.
Simba
 inatarajiwa kushuka Uwanja wa Uhuru Novemba 24 kumenyana na Ruvu 
Shooting mchezo wao wa 10 kwenye ligi ikiwa nafasi ya kwanza baada ya 
kucheza mechi 9 na imejikusanyia pointi 22, imepoteza mchezo mmoja mbele
 ya Mwadui FC na imeshinda mechi saba na sare moja dhidi ya Prisons

0 comments:
Post a Comment