Mtibwa
Sugar walikuwa wa kwanza kutinga hatua hiyo kwa ushindi wa penalti 4-2
walioupata mbele ya Yanga baada ya dakika tisini kulazimisha sare ya bao
1-1.
Simba
nao walikuwa washindi wa nusu fainali ya pili mbele ya Azam FC kwa
ushindi wa penalti 3-2 baada ya dakika tisini kutoka sare ya bila
kufungana.
Azam FC ambao walikuwa mabingwa watetezi msimu huu watakuwa watazamaji wa fainali hii itakayopigwa Januari,13.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na timu zote kupania kutwaa taji la kwanza kwa mwaka 2020.
Kiungo
wa Mtibwa Sugar, Humud amesema kuwa mchezo mgumu ulikuwa dhidi ya Yanga
wana imani watapenya mbele ya Simba na kupata matokeo.
Kwa
upande wa Simba, mlinda mlango, Beno Kakolanya amesema kuwa wachezaji
wapo vizuri na wanaamini utakuwa mchezo mgumu ila watapabana kupata
matokeo.
0 comments:
Post a Comment