DAKIKA 12 za kiungo mpya wa Simba, Luis Miqoissone
akitokea benchi kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga zimemkosha Kocha
Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck ambaye alibaki akitikisa kichwa
kuonyesha kwamba amekubali uwezo wa nyota huyo.
Raia
huyo wa Msumbiji aliyetokea timu ya UD Songo na kusaini kandarasi ya
miaka miwili alikuwa na kasi ya kuitafuta mipira na kutoa pasi kwa
wachezaji wenzake kwa umakini.
Jezi
yake mgongoni ni namba 11 iliwahi kuvaliwa na mshambuliaji wa zamani
Laudit Mavugo na ilikuwa ikivaliwa na mbrazil, Wilker da Silva ndani ya
dakika 12 alizotumia kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi uwanja wa
Gombani dhidi ya Zimamoto alisababisha faulo mbili kutokana na kuchezewa
rafu na wachezaji wa Zimamoto .
Habari
kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa bado Sven anamvutia kasi nyota
huyo ili kuona ni namna gani ataweza kuingia kwenye mfumo wake mpya wa
kikosi chake cha kwanza.
Ushindi
wa mabao 3-1 dhidi ya Zimamoto umeipa nafasi Simba kutinga hatua ya
nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na leo itamenyana na Azam
FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali.
Kocha
Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa ni ngumu kuzungumzia
mchezaji huyo kwenye mechi ya kwanza kwani bado mechi zipo.
0 comments:
Post a Comment