
Real Madrid bado
inataka kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 30,
licha ya ajenti wake kutilia shaka uhamisho wake msimu wa joto.
(Telegraph)
Chelsea imeungana na Tottenham kumsaka winga wa
Ufaransa Thomas Lemar, 24, kwa mkopo kutoka Atletico Madrid hadi mwisho
wa msimu huu. (Telegraph)Manchester United wamekubali kuwa haitafanikiwa kumleta Old Trafford kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27. (Evening Standard)

Tottenham wamefikia mkataba wa £28m kumnunua mshambuliaji wa AC Milan na Poland Krzysztof Piatek, 24. (Sun)
Spurs wanamtaka beki wa Barcelona na Portugal Nelson Semedo, 26. (Mirror)

Leicester haijakatiza matumaini ya kumsajili beki wa Juventus na Uturuki Merih Demiral, 21, licha ya ofa zao mbili kukataliwa na pamoja na ushindani kutoka Manchester City. (Mirror)
Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Unai Emery amefichua kuwa Everton ilimhoji kwa saa tatu kuhusu usimamizi wa klabu hiyo kabla ya kumuajiri Carlo Ancelotti. (Mail)

Barcelona itamenyana na Arsenal kumsajili beki wa RB Leipzig na Ufaransa wa chini ya miaka -21 Dayot Upamecano, 21. (Express)
Tetesi Bora Alhamisi
Arsenal na Manchester United wamewasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32. (El Chiringuito - via Metro)
Manchester United wanaaminika kutaka kumsajili beki wa klabu ya Hellas Verona ya Italia na raia wa Albania Marash Kumbulla, 19. (Star)
Ajax wanapanga kumrudisha beki Matthijs de Ligt, 20, kwa mkopo licha ya kumuuza mchezaji huyo licha ya kumuuza Juventus mwishoni mwa msimu uliopita. (A Bola - in Portuguese)

Crystal Palace wamekataa kumuuza Zaha kwa vigogo wa Ujerumani Bayern Munich. (Guardian)
0 comments:
Post a Comment