JOSE
Mourinho, Kocha Mkuu wa Tottenham amesema kuwa hakuona msaada wa VAR
kwenye mchezo wao dhidi ya Liverpool kwani kuna kadi nyekundu ya moja
kwa moja ilipaswa itolewe kwa mchezaji wa Liverpool ambaye alicheza rafu
mbaya kwa mchezaji wake.
Kwenye
mchezo wa jana, Januari, 11, Liverpool ilishinda bao 1-0 lililopachikwa
kimiani na Roberto Firmino dakika ya 37 akimalizia pasi ya Mohamed
Salah ulikuwa na ushindani mkubwa kwa pande zote mbili.
Mourinho
amesema kuwa ilipaswa kitendo cha Andy Robertson kitazamwe kwenye VAR
ili apewe adhabu kutokana na kumchezea rafu Japhet Tanganga ila
haikufanyika hivyo jambo ambalo halina maana ya uwepo wa huo mtambo
inaonekana muda huo walikuwa wanakunywa chai.
Tottenham
imepoteza mchezo huo ikiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani waTottenham
Hotspurs ambayo ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza
mechi 22 huku Liverpool ikiwa namba moja na pointi 61 imecheza mechi 21.
Mwamuzi
wa mchezo huo Martin Atkison hakutoa nafasi kwa Spurs kucheza faulo
wala kufanya marudio kwenye VAR jambo lililomkasirisha bosi huyo kwa
kuwa kulikuwa na ulazima kwa msimamizi wa mitambo hiyo kusimamisha mechi
na kutoa adhabu ya faulo kwao.
Hasira
za Mreno huyo alikumbushia pia na mechi yake dhidi ya Chelsea wakati
faulo ya nyota wake Son Heung-min ilirudiwa alipomchezea Antonio
Rudiger wakati wakiambulia kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Chelsea,
Desemba 22,2019.
Robertson
mwenye miaka 25, alikuwa msaada mkubwa kwa Liverpool wakati wakiibuka
na ushindi huo wa kwanza kwenye uwanja mpya wa Tottenham na alicheza
dakika zote tisini.
"Kiuhalisia
walipaswa wamalize dakika tisini wakiwa na wachezaji 10 pekee kwenye
mechi yao dhidi yetu, nadhani watu wa VAR muda huo labda walikuwa
wanakunywa chai jambo lililowafanya washindwe kuona kadi nyekundu ambayo
alistahili kupewa Robertosn ," amesema.
0 comments:
Post a Comment