Thursday, January 9, 2020



LUC Eymael, Kocha Mkuu mpya wa Yanga amesema kuwa anafurahi kujiunga na kikosi hicho kwenye benchi la ufundi.

Eymael ametua Bongo leo na atajiunga na klabu ya Yanga baada ya kumaliza taratibu za mwisho.

Akizungumza mara baada ya kutua kwenye ardhi ya Bongo, Eymael amesema kuwa anaona fahari kujiunga na timu kubwa.

"Ni furaha yangu kuona kwamba nimepata timu kubwa ndani ya Afrika. Ninaitambua vema falsafa yake na namna ilivyo hivyo nina imani tutakwenda nayo sawa," amesema.

0 comments:

Post a Comment