NAHODHA Msaidizi wa
Yanga, Juma Abdul ambaye ni beki wa kulia amesema kuwa hawatishwi na
wapinzani wao Simba kuelekea kwenye mchezo wao utakaopigwa leo. Januari,
4 uwanja wa Taifa bali wanawaheshimu.
Abdul mwenye asisti
moja ndani ya ligi amecheza jumla ya mechi saba ambazo ni sawa na dakika
630 amekuwa kwenye ubora wake msimu huu baada ya kutoka kwenye majeraha
msimu uliopita.
Akizungumza na
Championi Ijumaa, Abdul alisema kuwa maandalizi yapo vizuri na kila
mchezaji amepewa majukumu yake ya kutimiza ili kufikia malengo ya kupata
ushindi.
“Tumekuwa bora kwa
sasa na kila siku kikosi na morali inaongezeka, kwa sasa hatuna mashaka
na mchezo wetu dhidi ya Simba tutapambana kupata matokeo chanya kikubwa
mashabiki watupe sapoti tunahitaji pointi tatu,” alisema.
Kwa upande wa Simba,
beki kisiki Pascal Wawa ambaye amecheza jumla ya mechi tisa sawa na
dakika 810 amesema kuwa hawana hofu na mchezo wao dhidi ya Yanga.
“Kama siku zote
ambavyo huwa tunafanya kutazama mbele na kutafuta matokeo, kila mchezo
ni muhimu kwetu kushinda, tunaamini katika Mungu na jitihada, mashabiki
watupe sapoti,” alisema Wawa.
Simba iliyo nafasi
ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 13
itakuwa mwenyeii wa Yanga iliyo nafasi ya tano baada ya kucheza mechi 11
ikiwa na pointi 24 kibindoni.
0 comments:
Post a Comment