KOCHA
Mkuu wa Wolves, Nuno Espirito Santo amesema kuwa mshambuliaji wake Raul
Jimenez anaweza kusepa ndani ya klabu hiyo mwezi huu na kujiunga na
Manchester United.
Habari
zinaeleza kuwa Manchester United wanahitaji saini ya nyota huyo ambaye
amekuwa kwenye ubora wake ili kuongeza ukali wa safu yao ya
ushambuliaji.
Raia
huyo wa Mexico alitokea benchi kwenye mechi ya FA jana, Jumamosi ambapo
Wolves ililazimisha sare ya bila kufungana mbele ya United raudi ya
tatu.
Jimenez
amefunga jumla ya mabao 17 na pasi tisa za mabao kwenye jumla ya mechi
zake zote 32 alizocheza akiwa na Wolves kwenye mashindano yote msimu
huu.
0 comments:
Post a Comment