
Napoli na Ajax ziko
tayari kumpigania Jan Vertonghen, 32, na kuishawishi Tottenham kumuuza
beki huyo raia wa Ubelgiji kabla ya kuruhusiwa kuondoka kwa uhamisho wa
bure msimu wa joto. (Telegraph)
Marseille na Aston Villa ni
miongoni mwa klabu zinazomfuatilia mshambuliaji wa Liverpool Daniel
Sturridge, 30, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Uturuki ya
Trabzonspor. (Mail)Real Madrid imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 27. (Le10Sport)

Kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 27, atalazimika kusubiri mkufunzi wa Arsena Mikel Arteta kutafakari pendekezo lake la kuhamia Hertha, Berlin kwa mkopo mwezi huu wa Januari. (Independent)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amedokeza kuwa kiungo wa kati wa England Adam Lallana, 31, huenda akaondoka katika klabu hiyo pindi mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu huu. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 25, ambaye alikuwa akilengwa na Manchester United, amesema anakaribia kujiunga na Tottenham msimu wa joto kuliko klabu nyingine yoyote. (Express)

0 comments:
Post a Comment