
Hatma ya beki John
Stones huko Manchester City bado haijafahamika lini atafungua mazungumzo
juu ya mkataba mpya, mkataba wa sasa umebakisha miaka miwili. (Sunday
Express)
Tottenham wamejipanga kuwapiku West Ham kumsaini kiungo wa Benfica Gedson Fernandes, 21, kwa mkopo wa miezi 18. (Sunday Mirror) Kiungo wa Ajax na Uholanzi Donny van de Beek amehusishwa na kuhamia Manchester United lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.(Fox Sports Netherlands, via ESPN)
Klabu ya Wolves inanafasi kubwa ya kumsaini Thomas Lemar wa Atletico Madrid kwa sababu ya uhusiano muzri wa Klabu hiyo na wakala wa mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye miaka 22, Jorge Mendes.
(Mundo Deportivo, via Sport Witness)


Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameonyesha nia ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 22. (ElDesmarque - in Spanish)
Sheffield United wanamfuatilia mlinzi wa kati wa Ipswich Town mwenye umri wa miaka 21, Luke Woolfenden, na klabu hiyo inampango wa kuwasaini mabeki wa kati wawili.(Sheffield Star)

Aston Villa na Newcastle United wako kwenye mapambano ya kumsaini mshambuliaji wa Le Havre Tino Kadewere, Norwich City na Tottenham pia wameonyesha kuvutiwa na mshambuliaji huyo wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka 24. (Football Insider)
Klabu ya Ufaransa Lyon pia wapo kwenye mapambano ya kujaribu kumsaini Kadewere.(Eurosport France, via Birmingham Mail)
Mshambuliaji wa Kiingereza wa Crystal Palace, Connor Wickham, 26, anatarajiwa kujiunga na Sheffield Jumatano kwa mkopo kufuatia kuwasili kwa Cenk Tosun, 28, katika uwanja wa Selhurst Park. (Mail on Sunday)

Manchester United wanashindana na kiungo wao wa zamani David Beckham mmiliki Inter Miami kwa kumsaini kiungo wa Boca Juniors na timu ya tiafa ya Argentina mwenye chini ya umri wa miaka 20 Agustin Almendra, (Star on Sunday)
Bosi wa West Ham United David Moyes anataka kumuongeza mlinzi wa zamani wa Everton Alan Stubbs kwenye timu yake ya makocha.(Star on Sunday)
0 comments:
Post a Comment