Wednesday, February 5, 2020


Rais wa Nigeria Muhammad Buhari amemtangaza rasmi kuwa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na kocha msaidizi wa timu hiyo Daniel Amokachi kuwa balozi wa soka la Nigeria, ambapo atakuwa na jukumu la kuendeleza na kulitangaza soka la Nigeria ikiwemo kuvumbua vipaji kupitia wizara husika.

Amokachi ,47, alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria cha 1994  ambacho kilishinda michuano ya mataifa ya Afrika nchini Tunisia (AFCON), pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Olympic  cha Nigeria 1996 na kushinda medali ya dhahabu.

Kabla ya kustaafu Soka Daniel Amokachi aliwahi kucheza vilabu mbalimbali Ulaya kama vile Everton ya England na Club Brugge ya nchini Ubelgiji.

0 comments:

Post a Comment