Katika
hali ambayo sio ya kawaida shabiki mmoja wa klabu ya Newcastle alinaswa
na kamera za uwanjani akishangilia ushindi ambao timu yake umeupata
dhidi ya Oxford Unted kwa kutoa ‘nyeti’ zake nje kwenye mchezo wa raundi
ya nne michuano ya kombe la FA Cup.

Shabiki huyo alifanya tukio hilo hapo jana siku ya Jumanne mara baada ya mchezaji wa Newcastle, Allan Saint-Maximin kufunga goli la tatu na la ushindi dakika ya 116, baada ya timu hizo kwenda sare ya mabao 2 – 2 mpaka dakika 90.

Tukio hilo liliwashitua mashabiki wengi uwanjani baada ya kuliona kupitia TV, ambapo kijana huyo alionekana akifungua zipu yake ya jinzi kisha kutoa ‘nyeti’ zake kwa furaha baada ya timu yake kupata ushindi huo.

Baada
ya kutoa nyeti zake alionekana akiigiza kama anafanya ‘masturbation’
wakati klabu yake ya Newcastle ikisonga mbele kwenye uwanja huo wa
Kassam Stadium.
Kitendo hiko kimezua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii ya Twitter kiasi kwamba kila mtu amekuwa akifanya mzaha.
Mmoja akisema shabiki huyu wa Newcastle amefurahia sana goli, wakati mwengine akisema huo ndiyo uchawi wa michuano hiyo.
Bao
hilo la dakika za mwisho la Saint-Maximin linaifanya Newcastle kukutana
na West Brom katika mchezo ujao wa FA Cup utakao pigwa mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment