Wednesday, February 5, 2020


Nahodha wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amezua gumzo mitandaoni baada ya kuonyesha kukasirishwa na kauli ya Mkurugenzi wa Barcelona, Erick Abidal kwa kuwashutumu wachezaji wa Barcelona akisema kwamba walikuwa  hawajitumi kwa bidii kipindi cha kochaa Ernesto Valverde.

Messi amejibu kwa kumtaka Abidal atoe majina ya wachezaji hao vinginevyo anachafua jina la kila mchezaji na uvumi ambao sio kweli.
Maneno ya Abidal yalikuwa:- “Wachezaji wengi hawakuwa na furaha na hawakufanya kazi kwa kujituma na kulikuwa na shida ya mawasiliano ya ndani ndani kwa wachezaji,”
“Urafiki kati ya makocha na chumba cha kubadilishia nguo (Wachezaji) kuna kipindi ulikuwa mzuri, lakini kuna mambo nikiwa kama mchezaji wa zamani niliweza kuyaelewa. Niliiambia klabu kile nilichofikiria na tunapaswa kufanya uamuzi.”

Baada ya kauli hiyo ya Abidal Messi alitoa maoni yake kupitia ukurasa wake  wa Instagram akiweka kwenye Insta story akiwaambia maafisa wakuu wa Klabu hiyo kufanya majukumu yao na akawatahadharisha dhidi ya kutaja baadhi ya wachezaji wakisema kuwa hakukuwa na maelewano kwa baadhi ya watu.
“Kwa kweli sikupenda kufanya jambo la aina hii lakini nadhani kila mtu anapaswa kuwajibika kwenye kazi yake na kuchukua maamuzi katika uelewa wake”
“Wachezaji wanatakiwa kuwajibika kwa kile kinachotokea uwanjani na huwa tuko tayari kuwajibika na kutatua endapo kunakuwa na matatizo juu yetu, kwa wote ambao wanaisimamia hii timu wanatakiwa kuchukua maamuzi na kusimamia kile wanachokisimamia”
Mwisho kabisa niombe katika kila kitu ambacho kimetokea na wachezaji wamehusishwa inafaa kutajwa majina yao kwa sababu kama haitafanyika hiyo tutaonekana wote wachafu na tuna matatizo kwa kile kinachoongelewa kumbe sio kweli”


0 comments:

Post a Comment