
Eriksen amejiunga na miamba hiyo ya Serie A, mwezi uliyopita kwa dau la paundi milioni 6.9 ikiwa ni kandarasi ya miaka minne na nusu baada ya mkataba wake na Spurs kuelekea ku- ‘expire’ kipindi cha majira ya joto.
Nyota huyo wa Denmark, aliweza kuisaidia Tottenham kutinga hatua ya fainali ya Champions League na kutolewa na Liverpool lakini pia walitinga League Cup mwaka 2015.

“Hapa kunanafasi kubwa sana ya kushinda mataji, nafasi kubwa kuliko hata kule nilipokuwepo mwanzo.” Amesema Eriksen.
Christian Eriksen ameongeza “Usiku wa fainali ya Champions League ilikuwa siku mbaya sana, tulipoteza mchezo, tusingependa hata kukumbuka.”
“Nipo hapa kwaajili ya kushinda, na kuanza kitu kipya. Mara ya mwisho kushidna taji ilikuwa dhidi ya Ajax miaka mingi iliyopita. Bado nazikumbuka hisia zile za ushindi nahitahi kufanikiwa hilo nikiwa hapa pia.”
Wakati wa dirisha la usajili, Eriksen alihusishwa na kujiunga na klabu kadhaa zikiwemo na Real Madrid na Barcelona.
0 comments:
Post a Comment