”Bila shaka, tumejionea leo wote ‘game’ ilikuwa nzuri na yenye ufundi zaidi. Lakini mwisho wa yote tunamuachia Mwenyezi Mungu ndiye aliyepanga matokeo yawe hivi.” Kauli ya kocha wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini akizungumza na waandishi wa habari Uwanja wa Taifa baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Malale Hamsini akijibu maswali ya waandishi ameongeza kuwa ”Ni kweli tulitakiwa kumaliza ‘game’ mapema lakini kilichotushinda ni uzoefu tu, lakini mechi ilikuwa nzuri na vijana wangu walijituma zaidi.”
”Chumba chetu kilizimwa umeme, sasa hatujui nini tatizo.” Alimazima Kocha wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini ambaye alichukua nafasi ya Seleman Matola aliyetimkia Simba SC.
Kwenye mchezo huo Polisi Tanzania ilijikuta ikipoteza kwa kipigo cha magoli 2 – 1 mbele ya Mnyama mkali Simba.

Hata hivyo mechi hiyo imegubikwa na lawama kutoka kwa mashabiki na baadhi ya wachambuzi wa soka nchini wakidai bao la kwanza la Simba SC lilikuwa ‘offside’ kutoka kwa John Bocco.
0 comments:
Post a Comment