
Mmisri
huyo kwa sasa ndiyo aneye ongoza kwa idadi ya mabao ndani ya Liverpool
kwa mashindano yote msimu huu akiwa amejikusanyia jumla ya magoli 18.
Akiwa amewasaidia kupata ubingwa wa Champions League na sasa yupo katika
mbio za taji la Premier League.
Salah
pia ameifungia Liverpool zaidi ya mara tatu kwenye michezo yake miwili
ya mwisho, lakini, Bent anaamini Sadio Mane na Roberto Firmino
wanathamani kubwa kwa upande wa kocha, Jurgen Klopp.

Bent ameuambia mtandao wa ‘talkSPORT’ kuwa tatizo Mo Salah ni mbinafsi na hiyo ndiyo tafauti yake na nyota hao wengine wawili.
”Ukiangalia uchezaji wake kwa jumla, ukamlinganisha na Mane, naweza kusema Mane ni bora zaidi yake.” – Amesema Bent
”Anaweza
kufunga mabao mengi zaidi ya Mane, lakini kiwango cha Mane katika
ushiriki wake na timu uwanjani ni kikubwa. Hana ubinafsi yeye
huwaangalia wengine kwanza, hivyo huwezi kumuuza Mane ni muhimu sana kwa
timu.”
”Firmino, tunafahamu hafungi
sana magoli, lakini yeye ndiyo mpishi anaye watengenezea wenzake, kiungo
anaye waunganisha wachezaji.”
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa England, alimalizia kwa kumtaka Klopp kuto kuwa na
hofu linapokuja swala la kuuzwa kwa Salah, kama endapo tu anaweza
kumleta kikosini Mbappe ama Sancho.
Je msomaji umeupokeaje ushauri wa Darren Bent kwa Liverpool ?
0 comments:
Post a Comment