KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck ameshikilia hatma ya nyota wake Shiza Kichuya kucheza kwa sasa ndani ya kikosi hicho.
Kichuya ambaye ni kiungo mshambuliaji wa Simba alikuwa anashugulikia suala la kibali cha kucheza soka ndani ya Bongo.
Taarifa
rasmi iliyotolewa na Uongozi wa Simba imeeleza kuwa hatma ya Kichuya
kwa sasa kucheza ndani ipo mikononi mwa Kocha Mkuu, Sven Vanderbroeck.
Kichuya
alisajiliwa na mchezaji mwingine Luis Miquissone aliyekuwa akikipiga UD
Songo yeye taarifa zinaeleza kuwa bado ITC yake haijatolewa na Simba
wamepeleka suala hilo kwenye Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ya FIFA.
Kichuya
ambaye alikuwa mchezaji wa Simba na alijipatia umaarufu kwa kufunga bao
la kona wakati Simba ikicheza na Yanga msimu wa 2016/17 na ngoma
iliisha 1-1.
Alikuwa
akikipiga ndani ya Klabu ya Ennpi ya Misri inayoshiriki Ligi Kuu nchini
Misri, alirudishwa tena ndani ya Simba kwenye dirisha dogo la usajili
wa msimu huu hakupata nafasi ya kutumika kwenye mechi nne za Ligi Kuu
Bara ambazo zilichezwa hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment