Ni
maoni yangu kama Mdau wa Michezo na Mwandishi wa Habari za Michezo
kutoka Tanzania, kwa Soka letu lilipofikia sasa na utata wa maamuzi
uliopo katika Soka hili la Bongo, sina shaka wala ubishi tuifikirie
Video Assistant Referee (VAR) ijapokuwa ni gharama kuiendesha.
Kwa hakika VAR itatusaidia kufika mbali na itawasaidia
Waamuzi wetu wanaochezesha Soka lenyewe, naamini pia itaondoa utata na
hata kupunguza makosa hasa wanayokutana nayo Waamuzi wanaoamua michezo
mbalimbali hususan ile ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL).
Kama
tunavyoona ulimwenguni katika Dunia ya kwanza namaanisha barani Ulaya,
VAR imeondoa utata kwa kiasi kikubwa kwenye michezo ya Ligi mbalimbali
zikiwemo Ligi maarufu na bora duniani Ligi Kuu za Uingereza (EPL),
Hispania (La Liga) na nyingine nyingi tu.
Sina
shaka wala hakuna ubishi kumekuwa na manung'uniko kwa baadhi ya Wadau wa
Soka nchini kuwa VAR inaondoa uhondo katika mchezo, la hasha hili
tusiliangalie wala kulitilia maanani sana. Kwa wenzetu wa Dunia ya
kwanza (Ulimwenguni) wanaitumia VAR kama kawaida bila kujali kupoteza
muda wala kuondoa uhondo wa mchezo husika, Je sisi ni akina nani
tunaopinga hili?
Naendelea kusema na kuwaza kwa
Mamlaka husika zinasosimamia mchezo wa Mpira wa Miguu nchini, VAR kwa
Soka letu la Tanzania tuifikirie ijapokuwa ni gharama kuitumia katika
mchezo mmoja. Sijui pengine baadae tunapoendelea tunaweza kuona umuhimu
wake licha ya gharama zake lakini bado nawaza nakusema tuifikirie basi
hata kwa michezo muhimu ya Ligi lakini michezo yote ya Ligi Kuu ni
muhimu.
Utata wakuamua OFFSIDE kwa Waamuzi
wetu, Mashabiki wa Soka wanasema ni Sheria mojawapo ya Soka ngumu zaidi
katika zile Sheria 17 za Soka zilizowekwa na Shirikisho la Kandanda
Ulimwenguni (FIFA), kwa hakika huenda ikawa kweli ni Sheria ngumu
kuitafsiri kwa Waamuzi wetu lakini kwa wenzetu (Ulaya) wanasaidiwa na
VAR kutatua changamoto hiyo ya tafsiri ya Sheria hiyo wao wanaangalia
pande (Angle) zote kuhakikisha kama ni Offside au la.
Utata
mwengine ni MAGOLI yanayofungwa bila kugusa Nyavu yaani kuvuta mstari
wa goli, hii nayo ni sehemu nyingine ya utata katika Soka letu la
Tanzania, lakini kwa wenzetu hakuna utata huo, VAR lazima ichukue nafasi
kuwasaidia Waamuzi, kwa kweli inapendeza mnoo.
Sijajua
kwa Ligi kubwa barani Afrika hasa kule Uarabuni kama kuna matumizi ya
VAR lakini mwaka jana tulishuhudia moja ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa
Afrika (CAF Champions League) kati ya Esperance de Tunis ya Tunisia na
Wydad Casablanca ya Morocco ambapo ulizuka utata mpaka Bingwa wa
Michuano hiyo kushindwa kupatikana kwa wakati, Fainali iliyopigwa mwezi
May, Bingwa kutangazwa mwezi August mwaka 2019.
Kwa
maoni yangu, VIDEO ASSISTANT REFEREE ikija nchini na hata barani Afrika
kwa ujumla nadhani Utata wote utaisha katika Soka letu na hata zile
shutma za Waamuzi wetu hazitakuwepo wala kupata nafasi bila kujali
kuondoa uhondo wa mchezo wa Soka nakupoteza muda.

0 comments:
Post a Comment