Thursday, February 6, 2020


Son Heung-min akishangilia baada ya kuifungia Tottenham Hotspur bao la ushindi dakika ya 88 kwa penalti ikiilaza 3-2 Southampton na kutinga Raundi ya Tano ya Kombe la FA England Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London. Mabao mengine ya Spurs yamefungwa na Jack Stephens aliyejifunga dakika ya 12 na Lucas Moura dakika ya 78, wakati ya Southampton yalifungwa na Shane Long dakika ya 34 na Danny Ings dakika ya 72

0 comments:

Post a Comment