ZINEDINE
Zidane, Kocha Mkuu wa Real Madrid amesema kuwa, Pep Guardiola ni
miongoni mwa makocha bora anaowaheshimu kutokana na kazi zao
wanazozifanya.
Real Mdardi na Manchester City zitakuwa kazini leo Uwanja wa Bernabeu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Amekuwa
bora kwenye timu nyingi ambazo amefundisha alikuwa Barcelona kisha
Munich na sasa yupo na Manchester City kwa maoni yangu, yeye ni kocha
bora wengine watafikiria kumtaja kocha mwingine.
"Kiukweli
ninapenda kile anachokokifanya na ninapenda kazi yake kwani
ananishawishi nami pia kwenye utendaji wangu wa kazi. Kwa namna ambavyo
ninajifunza kwake sina hofu ya kushuka uwanjani kukutana na timu yake
ama kucheza naye kwa kuwa ni mtu ninayemkubali,"amesema.

0 comments:
Post a Comment