KIPA
wa Simba, Aishi Manula amesema kuwa mchezaji wa zamani wa klabu hiyo,
Emmanuel Okwi ni mchezaji bora kuwahi kutokea katika klabu hiyo na bado
ana nafasi ya kurudi tena na kufanya vizuri kwani pengo lake halijawahi
kuzibika.
Manula amesema kila mchezaji ndani ya klabu hiyo ana
ubora wake, lakini Okwi ni mchezaji wa kipekee kuwahi kuichezea Simba,
kwani alifanya mambo makubwa na kucheza kwa kiwango cha juu kwa muda
wote aliovaa jezi ya timu hiyo.
Okwi alijiunga
na Simba kwa mara ya kwanza 2010 akitokea Sc Villa, kisha akatimka 2013
na kwenda Etoile du Sahel, kisha SC Villa, Young Africans, kisha 2014
akarudi tena Simba.
Akaondoka 2017 kwenda
SønderjyskE ya Denmark, akaenda Sc Villa na kurudi tena Simba 2017 na
2019, akatua Al Ittihad Alexandria Club ya Misri.
Akizungumzia
ishu hiyo Manula alisema: “Pengo la Emmanuel Okwi haliwezi kuzibika
kirahisi kwenye kikosi chetu na bado tunahitaji huduma yake. Lakini siyo
kwamba waliopo sasa hawana ubora bali kila mchezaji ana ubora wake na
ubora wa Okwi ni tofauti na ubora wa mchezaji mwingine yeyote, hivyo
hakutatokea mbadala wake,”
0 comments:
Post a Comment