
Winga wa kimataifa wa Ujerumani na Manchester City Leroy Sane, 24, anakaribia kuhamia Bayern Munich kwa kiasi cha £70m.(Mirror)
Klabu
za Ligi ya Premia zitakutana Ijumaa kujadili uwezekano wa msimu huu
kumalizika Juni 30. Ikiwa uamuzi huo utaamuliwa kwa kura, basi klabu 14
kati 20 zitahitajika kukubaliana. (Guardian)Kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, amedokeza kuwa yuko tayari kuhamia ughaibuni, huku Liverpool ikiwa ni miongoni mwa klabu ya Ligi ya Primia inayomtaka. (Sport Bild - in German)

Beki wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, 30, anataka kurefusha mkataba wake wa sasa wa mkopo nyumbani kwa Estudiantes kwa sababu amecheza mara moja tu na kujeruhiwa kabla ya ligi kusitishwa katokana na mlipuko wa vurusi vya corona. (Manchester Evening News)

Arsenal inatarajiwa kamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette mwisho wa msimu, huku Atletico Madrid wakipigiwa upato kumnunua kiungo huyo wa miaka 28. (AS - in Spanish)
Arsenal wanakaribia kukamilisha uhamisho wa bure wa beki wa Ufaransa wa miaka 27 Layvin Kurzawa kutoka Paris St-Germain.(Daily Star)


Kipa wa Liverpool Loris Karius amesema bado anawasiliana na Jurgen Klopp, japo yuko klabu ya Uturuki ya Besiktas, hana uhakika kuhusu hatima yake ya baadae. Mkataba wa Mjerumani huyo wa miaka, 26, Anfield unaendelea hadi 2022. (Sky Sports)
0 comments:
Post a Comment