
Newcastle imeanza
mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho,
28, baada ya Bayern Munich kubadili nia ya kumpatia mkataba wa kudumu
nyota huyo wa kimataifa wa Brazil. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Magpies
pia wanamlenga kiungo wa kati wa Liverpool Xherdan Shaqiri, 28, dirisha
la uhamisho wa wachezaji litakapofunguli tena msimu wa joto. Kiungo
huyo wa kimataifa wa Uswizi amewakilisha klabu hiyo mara 10 tu msimu
huu. (Mail)
Arsenal na Tottenham wanang'ang'ania kumsajili kwa mkataba wa bila malipo kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 31, ambaye mkataba wake Stamford Bridge unakamilika msimu huu. (Telegraph)
Wolves huenda wakamnunua kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Joao Palhinha, 24. (Mirror)

Klabu ya Portugal ya Vitoria Guimaraes inataka kumnunua mchezaji kinda wa Crystal Palace Jadan Raymond, 16, kwa £250,000 kandarasi yake ikielekea kumalizika mwisho wa mwezi ujao. (Sky Sports)
Tetesi za soka Jumanne
Everton imewasilisha ombi la £40m kumsaini kiungo wa kati wa Napoli, Allan, 29, lakini klabu hiyo inataka dau la £60m kumuuza raia huyo wa Brazil. (Il Mattino - in Italian)
Mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Mauro Icardi, 27, anakaribia kuhamia katika klabu ya Paris St-Germain kwa dau la £54m. (ESPN)

0 comments:
Post a Comment