
Chanzo cha picha, Getty Images
Pierre-Emerick Aubameyang alifunga goli zuri na kuongeza bao jingine la penalti na kuisadia Arsenal kuilaza miamba ya ligi ya Uingereza Liverpool katika kombe la Community Shield katika mechi iliochezwa katika uwanja wa Wembley bila mashabiki.
Mshambuliaji wa Liverpool Rhian Brewster alieingizwa kunako dakika za mwisho alipiga mwamba wa goli na kuisaidia Arsenal kushinda taji hilo.
Shambulio la Aubemayenga lililojipinda liliwapatia mabingwa hao wa kombe la FA uongozi katika kipindi cha kwanza kabla ya gusa niguse ya mchezaji wa ziada Minomino na Mohammed Salah kusawazisha .
Uchunguzi wa VAR ili kubaini iwapo huenda kulikuwa na kasoro katika ufungaji wa goli hilo haukusema kwamba Salah alikuwa ameunawa mpira.
Ni mwaka wa pili mfululizo Liverpool imepoteza kwa njia penalti baada ya ushindi wa Manchester City mwaka 2019.
Aubameyang aiongoza Arsenal kushinda mataji zaidi
Umuhimu wa Aubameyang katika klabu ya Arsenal kwa mara nyengine ulionekana baada ya kuonesha mchezo wa kuvutia .
Mchezaji huyo raia wa Gabon aliyefunga mara mbili katika kombe la FA katika uwnaja huohuo mwezi huu aliingia kutoka upande wa kushoto na kushambulia katika kona ya mkono wa kushoto wa kipa .

Naohodha wa kikosi cha Arsenal Emerick Aubameyang
Aliendelea kufanya mashambulizii katika safu ya ulinzi ya Liverpool huku beki wa kulia Necco Williams akishindwa kumzuia.
Na Aubameyang alipojitokeza kupiga penalty ya mwisho huku magoli yakiwa 4-4 hakuna njia ambayo ingemzuia kufunga goli hilo.
Amefunga magoli 71 katika mechi 110 alizochezea Arsenal na hakuna mchezaji yeyote wa Arsenal amefunga magoli zaidi ya yake matano katika uwanja wa Wembley.
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta siku ya Ijumaa alisema kwamba ana imani kwamba nahodha huyo wa Arsenal ataandikisha kandarsi mpya baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
Baada ya kushinda kombe la pili katika kipindi cha mwezi mmoja, utakuwa msimu mzuri wa Arsenal iwapo Aubameyang atatia kandarsi mpya.

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool washindwa kufurukuta kwa mara nyengine
Liverpool hawakuwa na wachezaji wao wa kikosi cha kwanza Trent Alexander-Arnld na Jordan Hernderson lakini walianzisha kikosi ambacho wengi walihisi kinaweza kuilaza Arsenal.
Lakini walishindwa kufurukuta katika kipindi cha kwanza - huku Virgil van Dijk akiwalaumu Georginho Wijnaldum na Fabinho kwa kupaena mipira ovyo katika safu ya kati.

Sadio Mane alilazimika kurudi nyuma katika kipindi kirefu cha mechi ili kushirikiana na Andy Robertson.
Beki wa kulia wa Arsenal Ainsley Maitland -Niles alionesha umahiri mkubwa na kuisababishia matatizo huku Bukayo Saka akiwa na kazi kubwa katika safu ya ulinzi ya Liverpool.
Lakini Liverpool ilikuwa na nafasi chungu nzima ilizoshindwa kuzifanya magoli .
0 comments:
Post a Comment