BEKI
wa Manchester City, Joao Cancelo akishangilia baada ya kuifungia Ureno
bao la kwanza dakika ya 41 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Croatia kwenye
mchezo wa Kundi la Tatu Ligi ya Mataifa ya Ulaya usiku wa jana Uwanja
wa Do Dragao Jijini Porto. Mabao mengine ya Ureno iliyomkosa nyota wake,
Cristiano Ronaldo yalifungwa na Diogo Jota dakika ya 58, Joao
Felix dakika ya 70 na Andre Silva dakika ya 90 na ushei, wakati
la Croatia lilifungwa na Bruno Petkovic dakika ya 90
0 comments:
Post a Comment