Tuesday, May 30, 2017

details mei 30 2017
 Ernesto Valverde
 Barcelona wamemteua Ernesto Valverde kuwa mkufunzi wao mkuu kwa mkataba wa miaka miwili, ambapo anaweza akaongezewa mwaka mwingine wa tatu.
Valverde ni mshambuliaji wa zamani wa Barca na alitangaza wiki iliyopita kwamba angeacha kazi Athletic Bilbao baada ya kuwaongoza kwa miaka minne.
Anachukua nafasi ya Luis Enrique aliyetangaza Machi kwamba angeihama klabu hiyo iliyomaliza nafasi ya pili La Liga msimu huu.
Anaondoka baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu

0 comments:

Post a Comment