
Klabu za Huddersfield Town na
Reading leo zinatarajiwa kuchuana kwenye mchezo wa fainali ya Mechi za
Mchujo za Championship ili kupata timu moja itakayopanda kwenda Ligi
kuu ya England (Epl) kwa msimu ujao .
Mpaka sasa Newcastle na
Brighton, zilishapanda moja kwa moja kwa kumaliza nafasi za kwanza na
ya pili kwenye Ligi na nafasi ya 3 hupatikana kwa Mechi za Mchujo
unaoshirikisha Timu za nafasi ya 3 hadi 6, Kwenye Championship, Reading
ilimaliza nafasi ya 3 na Huddersfield nafasi ya 5.Huddersfield imefikia Fainali hii kwa kuishinda Sheffield Wednesday waliyotoka 0-0 Mechi ya Kwanza na kisha sare nyingine ya 1-1 na Huddersfield kutinga Fainali kwa Penati 4-3, Reading wao waliwabwaga Sheffield Wednesday 1-0 baada ya Sare ya 1-1 katika mechi ya Kwanza.
Mshindi wa Leo, pamoja na Newcastle na Brighton, zitazibadili Hull City, Middlesbrough na Sunderland ambazo tayari zimeshushwa Daraja
0 comments:
Post a Comment