Wednesday, May 31, 2017


  mei31  2017
 by alanus

Awali Tiger Woods alikanusha kulewa akiwa anaendesha gariSiku moja baada ya mchezaji nyota wa gofu Tiger Woods kukausha kuwa hakuwa amelewa wakati polisi walipomkamata siku ya jumatatu, taarifa za polisi zinasema kuwa mchezaji huyo alikutwa amelala ama (amezima) wakati injini ya gari ikiwa inafanya kazi.

Tiger Woods akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa
Tiger Woods: Sikuwa nimekunywa pombe
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Woods mchezaji wa zamani namba moja kwa ubora duniani, alikutwa katika usukano wa gari yake aina ya Mercedes na aliamshwa kwa dakika kadhaa na afisa wa polisi aliyemuona.
Alikamatwa kwa kosa la kuendesha chombo cha moto akiwa amelala lakini alikanusha hilo na kusema kuwa ni matokeo ya dawa kali anazozitumia baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo.

0 comments:

Post a Comment