Thursday, June 14, 2018


Moja kwa moja
Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 inaanza leo Alhamisi nchini Urusi. Tunakuletea taarifa za moja kwa moja kuhusiana na mashindano hayo.

Muhtasari

  1. Michuano hiyo itashirikisha mataifa 32, wakiwemo mabingwa watetezi Ujerumani
  2. Kutakuwa na mechi 64 zitakazochezwa katika kipindi cha siku 32.
  3. Mechi ya kwanza itakuwa Urusi v Saudi Arabia na itachezwa baada ya kufanyika kwa sherehe ya ufunguzi katika uwanja wa Luzhniki, mjini Moscow.
  4. Mechi hiyo itaanza saa 12 jioni Afrika Mashariki
  5. Afrika itawakilishwa na mataifa matano Urusi: Nigeria, Misri, Senegal, Morocco na Tunisia

Habari za moja kwa moja

Maafisa wa usalama wa UrusiSerikali ya Urusi imeweka mikakati kuzuia na kukabiliana kwa haraka na visa vyovyote vya mashambulio ambavyo huenda vikatokea.
Moja ya tishio ni fujo za mashabiki, hasa kutokana na uhasama kati ya Urusi na England.
Kuna pia wasiwasi wa mashambulio ya kigaidi kutokana na Syria kushiriki vita Syria.
Katika kituo kikuu cha kufuatilia ulinzi Kaliningrad, kuna makundi maalum ya maafisa wa kufuatilia picha kutoka kwa kamera za CCTV.
Kuna kamera zaidi ya 700 za aina hiyo mjini humo, na nyingine 1,200 ndani ya uwanja wa Kaliningrad, ambapo England watacheza na Ubelgiji 28 Juni.
Kwa kutumia teknolojia yakutambua nyuso za watu, watu wanachunguzwa mara moja kwa kuangalia pia hazina data ya polisi kuhusu wahalifu.
Maafisa pia wamefutwa jinsi ya kujibu shambulio la kigaidi. Mfano kuna kundi maalum kwa jina Spetsnaz la maafisa wanaoweza kutumia parachuti kuruka angani na kuingia ndani ya uwanja shambulio likitokea wakati wa mechi.

  • Share this post

    ‘Uhispania hawana wakati wa kumzungumzia kocha aliyefutwa Lopetegui’

    Getty Images
    Fernando Hierro
    Meneja mpya wa muda wa Uhispania Fernando Hierro amesema taifa hilo halina muda wa kuendelea kuangazia kufutwa kwa kocha Julen Lopetegui Jumatano, siku mbili kabla ya Kombe la Dunia.
    Lopetegui, 51, alifutwa kazi na wakuu wa soka Uhispania kwa kutowafahamisha kwa wakati kwamba alikuwa ameteuliwa kuwa meneja wa Real Madrid baada ya Kombe la Dunia.
    Lopetegui atachukua mikoba kutoka kwa Zinedine Zidane.
    "Tumefika hapa kupigania Kombe la Dunia,” beki huyo wa zamani wa Uhispania mwenye miaka 50 alisema.
    “Tuna nafasi nzuri sana na hilo ndilo tunalofaa kuangazia.”
    Uhispania wataanza kampeni yao kwa mechi dhidi ya Ureno Ijumaa.
    Hierro alimaliza uchezaji wake 2004-05 akiwa na Bolton ya Uingereza.

  • Share this post

    Wenyeji Urusi wataanza kwa ushindi dhidi ya Saudi Arabia?

    Michuano ya Kombe la Dunia ya Fifa ya mwaka 2018 inaanza leo nchini Urusi ambapo Urusi watacheza dhidi ya Saudi Arabia baada ya kufanyika kwa sherehe ya ufunguzi katika uwanja wa Luzhniki, mjini Moscow.
    Mechi hiyo itaanza saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki. Michuano hiyo itashirikisha mataifa 32, wakiwemo mabingwa watetezi Ujerumani, na itakuwa na mechi 64 zitakazochezwa katika kipindi cha siku 32.
    Fainali itachezwa 15 Julai.
    Fainali za sasa za Kombe la Dunia ambazo ni za 21 zitachezwa katika viwanja 12 katika miji 11 nchini Urusi, ambayo inapatikana eneo la upana wa maili zaidi 1,800. Kutokana na hili, kutakuwa na tofauti kubwa katika wakati mechi zinachezwa.

  • Share this post

    Hujambo!

    Hujambo na karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu Kombe la Dunia, michuano ambayo inaanza leo nchini Urusi.

    0 comments:

    Post a Comment