Friday, June 30, 2017




Details  alanus

 30 June 2017


 

 TANZANIA Leo huko Afrika Kusini imetoka Sare 1-1 na Mauritius katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi A la COSAFA CUP na kutinga Robo Fainali.
Matokeo hayo na yale ya Angola kutoka 0-0 na Malawi ndiyo yamewabeba Tanzania kubakia uongozini na Washindi wa Kundi A na hivyo kutinga Robo Fainali ambako watacheza na South Africa.
Mauritius ndio walitangulia kufunga Bao Dakika ya 67 kwa Bao la Perticots na Dakika 1 baadae Simon Msuva kusawazisha.
Kundi B, ambalo linaongozwa na Zimbabwe, zitamaliza Mechi zake Ijumaa.
FAHAMU:
Hii ni mara ya 3 kwa Tanzania kucheza Mashindano haya baada ya kushiriki yale ya 1997 na 2015.
Kundi B la Mashindano la 2017 COSAFA Castle Cup lina Nchi za Zimbabwe, Madagascar, Mozambique na Seychelles.
Nchi Wanachama wa COSAFA, South Africa, Swaziland, Botswana na Zambia wataanzia Hatua ya Robo Fainali ambapo South Africa itacheza na Mshindi wa Kundi A na Swaziland kucheza na Mshindi wa Kundi B wakati Botswana ikivaana na Zambia.
Mashindano ya COSAFA yalianzishwa Mwaka 1997 na Nchi za South Africa, Zambia na Zimbabwe kubeba Kombe mara 4 kila moja wakati Angola ikibeba mara 3 na Namibia mara 1.
COSAFA CUP
MSIMAMO:
Makundi
25/6     1       Tanzania 2-0
25/6     2       Mauritius 0-1 Angola                            
26/6     3       Mozambique 0-4 Zimbabwe              
26/6     4       Madagascar 2-0 Seychelles                
27/6     5         Malawi 0-0 Mauritius                          
27/6     6         Angola 0-0 Tanzania                            
28/6     7         Zimbabwe 0-0 Madagascar                
28/6     8         Seychelles 1-2 Mozambique              
29/6     9         Tanzania 1-1 Mauritius                            
29/6     10       Malawi 0-0 Angola                                  
30/6     11       Mozambique vs Madagascar            
30/6     12       Zimbabwe vs Seychelles
Robo Fainali
01/7   13           Botswana vs Zambia                            
01/7   14           Namibia vs Lesotho                              
02/7   15           South Africa vs Tanzania                
02/7   16           Swaziland vs Mshindi Kundi B      

0 comments:

Post a Comment