Details
Created: Friday, 23 June 2017 04:26
>LEO MAPUMZIKO HUKO RUSSIA!MABINGWA wa Dunia Germany na Chile Jana huko Saint Petersburg Stadium, Mjini Saint Petersburg Nchini Russia, walitoka Sare 1-1 katika Mechi yao ya Pili ya Kundi B la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara.
Matoke ohayo yameziacha Chile na Germany kufungana kwenye Kundi B wote wakiwa na Pointi 4 kila mmoja na kuongoza Kundi hilo huku Cameroon na Australia zikiwa na Pointi 1 kila mmoja baada nao kutoka Sare 1-1 hapo Jana katika Mechi yao wa Awali.
Jana Fowadi wa Arsenali Alexis Sanchez aliweka Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Chile alipofunga Bao lake la 38 baada kuipa Chile uongozi katika Dakika ya 6 kwa Bao ambalo lilitokana na kosa la Beki wa Germany Shkodran Mustafi ambae pia huchezea Arsenal kama Sanchez.
Germany walisawazisha Dakika ya 41 kwa Bao la Lars Stindl.
Leo ni Mapumziko huko Russia na Mashindano haya yatarejea Jumamosi kwa Mechi za Mwisho za Kundi A ambazo zitaanza wakati mmoja ambapo New Zealand watacheza na Portugal na Wenyeji Russia kuwavaa Mexico.
++++++++++++++++
MSIMAMO:

++++++++++++++++
Jumapili, Kundi B nalo litamaliza Mechi zao kwa Germany kucheza na Camerron na Chile kucheza na Australia.
Washindi Wawili wa Juu wa kila Kundi ndio watasonga Nusu Fainali.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Germany: Marc Andre ter Stegen, Mustafi, Hector, Ginter, Draxler, Goretzka, Stindl, Can, Sule, Kimmich, Rudy
Chile: Herrera, Isla, Medel, Beausejour, Jara, Diaz, Aranguiz, Hernandez, Vidal, Vargas, Sanchez
REFA: Alireza FAGHANI [Iran]
++++++++++++++++
FIFA KOMBE LA MABARA
Ratiba/Matokeo:
Hatua ya Kwanza
Jumamosi Juni 17
KUNDI A
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
Russia 2 New Zealand 0
Jumapili Juni 18
KUNDI A
Kazan Arena, Kazan
Portugal 2 Mexico 2
KUNDI B
Spartak Stadium, Moscow
Cameroon 0 Chile 2
Jumatatu Juni 19
KUNDI B
Fisht Stadium, Sochi
Australia 2 Germany 3
Jumatano Juni 21
KUNDI A
Spartak Stadium, Moscow
Russia 0 Portugal 1
Fisht Stadium, Sochi
Mexico 2 New Zealand 1
Alhamisi Juni 22
KUNDI B
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
Cameroon 1 Australia 1
Kazan Arena, Kazan
Germany 1 Chile 1
Jumamosi Juni 24
KUNDI A
Kazan Arena, Kazan
1800 Mexico v Russia
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
1800 New Zealand v Portugal
Jumapili Juni 25
KUNDI B
Fisht Stadium, Sochi
1800 Germany v Cameroon
Spartak Stadium, Moscow
1800 Chile v Australia
Hatua ya Pili
Nusu Fainali
Jumatano Juni 28
Kazan Arena, Kazan
2100 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [NF1]
Alhamisi Juni 29
Fisht Stadium, Sochi
2100 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [NF2]
Mshindi wa 3
Jumapili Julai 2
Spartak Stadium, Moscow
1500 Atakaefungwa NF1 v Atakaefungwa NF2
FAINALI
Jumapili Julai 2
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
2100 Mshindi NF1 v Mshindi NF2
0 comments:
Post a Comment