by alanus
” shukuru kwa kila jambo Mungu ndio mpaji”
Huu ni mmoja kati ya msemo mkubwa
sana katika lugha ya Kiswahili ambao huonesha au huitayarisha nafsi kuwa
na mtazamo chanya kiimani.
Kinyongo ni kitu kibaya sana katika maisha ya mwanadamu . Hupofusha ufahamu na kuweka mazingira ya uovu pasipo sababu ya msingi.
Haruna Niyonzima kwa miaka kadhaa
toka ajiunge na Yanga SC amesimama kama mchezaji kipenzi kwa wanayanga
na hata wadau wengine wa soka nchini. Hii imetokana na kipaji chake
(remarkable) uwanjani na haiba yake kiujumla.
Katika miaka sita aliyoitumikia
Yanga SC ameipa mafanikio mengi akishirikiana na wenzake ; vikombe 4 vya
ligi kuu 2012-13,2014-15,2015-16 na 2016-17.
Msimu wa 2013 aliibuka mchezaji
bora wa ligi kuu Tanzania bara ndio msimu ambao jina la Fabregas
liliposhika hatamu. Ubora wake uwanjani uliwafanya Tanga kujizolea
mashabiki kila kona ya nchi na nje ya nchi hususani nchini Rwanda
anapotoka kiungo huyu.
Niyonzima pia amesimama kama
sehemu ya nguzo imara kuipeleka Yanga SC hatua ya makundi kombe la
Shirikisho lakini muuanganiko wake na Thabani Kamusoko kwa mechi kadhaa
za klabu bingwa Afrika ukisimama kama kielelezo cha ubora wake. Mechi na
Al Ahly Misri na hapa nyumbani ni moja ya mechi ambazo utatamani kila
saa kuzitazama.
Vikombe vitatu vinne ngao ya jamii
na kombe moja la FA (ASFC ) ni vitu ambavyo vinakupa sababu ya kuinua
mikono juu na kusema asante.
Wakati Yanga SC wakicheza na FC
Platinum ya Zimbabwe, mmoja wa wachezaji ambao walionja joto ya jiwe ya
kiungo Thabani Scara Kamusoko ni Haruna Niyonzima. Jambo hilo lilimfanya
baada ya mechi kumkimbilia kocha mkuu wa Yanga SC wakati huo Hans Van
Pluijm na kumsihi kumwangalia kiungo huyo na kumsajili katika kikosi
chao jambo ambalo Hans aliridhia na kumsajili. Hii inaonesha mapenzi
makubwa aliyokuwa nayo mchezaji huyo kwa klabu yake.
Tunaweza kuchachua nyongo zetu leo
na kuamua kumchukia Haruna kisa anaondoka Yanga kwa klabu yake
kushindwa kufikia dau lake lakini kuna vitu lazima tujiulize kama
binadamu katika dhana ya ustaarabu wetu . Tuna haki ya kumchukia?
Mwaka 2009 Christian Ronaldo
alipohama Manchester United kwenda Real Madrid, mashabiki wengi wa Old
Traford waliumia sana lakini hawakumtupia lawama na mpaka leo amebaki
kama balozi wao mwema zaidi kilichotokea ni kuwavuta kuishabikia timu
hiyo ya Uhispania.
Haruna ana legacy kubwa kama
mchezaji wa kigeni aliyewahi kudumu kwa miaka mingi katika klabu ya
Yanga tena kwa mafanikio na hiki ndio kinawatesa wana Yanga SC na mbaya
zaidi kuhusishwa na kuhamia kwa mahasimu wao wakubwa Simba SC. Lakini
wanajangwani wanatakiwa kuelewa hili si jambo geni katika soka na kamwe
alistahili chuki zaidi ya kuinua mkono wa heri. Ni nani asiyetambua
mchango na thamani ya Lunyamila Yanga? lakini alivaa jezi ya msimbazi.
Kizota na mapenzi yake kwa Yanga alivaa jezi ya Simba, Mohamedi Hussein
moyo wa Yanga lakini pia alivaa uzi wa wekundu hao wa Msimbazi. Nemesi
mmoja wa magolikipa mahiri wa Yanga miaka ya 90, alitimkia Simba pia.
Wapo wengi sana.
Wanajangwani wanatakiwa kumwambia
Haruna ‘asante’ na kutizama jinsi gani ya kukiimarisha kikosi chao bila
yeye ili kulinda ubingwa wao na ufahari wao katika soka la Tanzania na
kujaribu mafanikio mazuri kimataifa.
Ni dhahiri hali ya kiuchumi
imemuondoa klabuni na sio usaliti wa aina yoyote kama ilivyokuwa kwa
watangulizi wake kama Mrisho Ngasa na wengineo ambao hata siku moja
hawakuwahi kuamini Yanga inaweza kuwappteza. Mpira ni ajira na biashara
yao acha watafute maisha ili tusije kuwalaumu baadae licha ya ubora wao
wanakufa masikini.
Hata mwaka 1994 mchezaji kipenzi
wa Yanga SC aliyedumu kwa miezi 8 tu! klabuni na kujizolea umaarufu
mkubwa kwa kipaji chake , Costantine Kimanda akiwa na mwenzake Ngadou
Ramadhani toka Burundi alipoamua kutumkia Uarabuni kusaka maisha bora
wengi waliumia lakini mpaka leo Yanga bado imesimama imara na
ikishikiria rekodi yake ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu mara nyingi
zaidi.
0 comments:
Post a Comment