details june1 2017
by alanus
Uhamisho wa kipa huyo mwenye umri wa
miaka 23 umeigharimu City kitita cha paundi milioni 35 na kumfanya kuwa kipa wa
pili ghali katika historia baada ya Gianliugi Buffon aliposajiliwa na Juventus
akitokea Parma mwaka 2001.
Ederson alisafiri kwenda Manchester
Jumatatu na Jumanne alitua katika uwanja wa mazoezi wa City kukamilisha vipimo
vya afya na kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya klabu.
City sasa wanakuwa wameshatumia
kitita cha paundi milioni 78, baada ya klabu hiyo kumsajili kumnasa kiungo
Bernardo Silva kwa kitita cha paundi milioni 43 kutoka Monaco.

0 comments:
Post a Comment