
by alanus
Bingwa mtetezi wa michuano ya tenesi
ya Aegon Muingereza Andy Murray, ametupwa nje ya michuano hiyo na
mchezaji namba 90 kwa ubora wa mchezo huo Jordan Thompson.
Murray anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango vya tenesi alifungwa kwa 7-6 (7-4) 6-2.
Stan Warrinka nae alitupwa nje ya michuano hiyo baada ya kuchapwa na Feliciano Lopez kwa seti mbili alizopoteza kwa 7-6 na 7-5.
Nyota mwingine aliyeondolewa kwenye michuano hiyo ni Milos Raonic aliyefungwa na Thanasi Kokkinakis kwa seti mbili ya 7-6 na 7-6.
0 comments:
Post a Comment