By alanus
RAIS wa Real Madrid, Florentino
Perez ameibuka na kuanza kumtetea Cristiano Ronaldo juu ya kashfa ya kukwepa
kodi inayomkabili, mara tu baada ya kutoka kwa habari za mchezaji huyo kutakiwa
na timu yake ya zamani, Manchester United.
Ronaldo amekuwa akihusishwa na
mpango wa kuondoka Bernabeu - huku uwezekano ukiwa ni kurejea kwa Mashetani
Wekundu - baada ya kupoteza furaha kutokana na kutopewa sapoti na Madrid juu ya
kesi yake kukwepa kodi.
Nahodha huyo wa Ureno anatuhumiwa
kuuza haki za picha zake kwa kampuni moja Uingereza na kukwepa kulipa kodi ya
Pauni Milioni 13 Hispania. Perez amesema anamfahamu Ronaldo ni mstaarabu,
ambaye hawezi kufanya hivyo.
Rais
wa Real Madrid, Florentino Perez amemtetea Cristiano Ronaldo juu ya kashfa
yake ya kukwepa kodi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Amesema wamejiridhisha kwamba wakati
wote Cristiano amekuwa akifanya mambo mema, kwa sababu namna alivyo.
"Wote tunatakiwa kutimiza
wajibu wetu wa kulipa kodi zetu,' amesema Perez na kuongeza kwamba Ronaldo
amekuwa akitumia kampuni ile ile aliyokuwa akiitumia England na hakuwa na
tatizo huko. Amesema pia mchezaji huyo hakujaribu kuficha chochote.
Alipoulizwa kama zilikuwa mbinu za
Ronaldo kutaka alipiwe faini na klabu ambayo inaweza kufika Euro Milioni 40,
Perez akasema: "Swali halina maana kwa sababu hayuko hivyo, kama hayuko
sawa, si kwa sababu hiyo. Sijazungumza naye tangu Cardif (Real ilipoifunga
Juventus 4-1 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya). Amekuwa na mawasiliano
nasi, hivyo ni mchezaji wa Madrid,".
Pamoja na hayo, Perez amesema
hajazungumza na klabu yoyote juu ya uhamisho wa mchezaji yeyote hadi sasa,
si Cristiano Ronaldo, ama Alvaro Morata, au James Rodriguez.
0 comments:
Post a Comment