
Timu ya taifa ya Ujerumani imeichapa
timu ya Australia kwa mabao 3-2 katika mchezo wa kundi wa kombe la
mabara michuano inayofanyika huko nchini Urusi.
Iliwachukua dakika
tano tu kwa Ujerumani kuandika bao la kwanza kupitaia mshambuliaji wa
ke Lars Stindl, Australia wakasawazisha goli hilo katika dakika ya 41
kwa goli la Tom Rogic.Mshambuliaji matata wa Ujerumani Julian Draxler akaongeza goli la pili kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 45.
Dakika ya 48 Ujerumani waliongeza bao la tatu kupitia kwa kiungo Leon Goretzka, goli la pili la Austaria lilifungwa na mshambuliaji Tomi Juric anayekipiga katika klabu ya FC Luzern.
0 comments:
Post a Comment