by alanus
Mshambuliaji
Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji kuanzia msimu ujao atavaa jezi
namba 10 katika kikosi hicho akiachana na namba 77 aliyokuwa akiivaa
tangu alipojiunga nao.
Samatta
ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars, amekuwa akivaa jezi namba 10 pia
katika kikosi cha timu ya taifa lakini tangu alipojiunga na Genk mwaka
jana amekuwa akivaa jezi namba 77.
Katika
taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Genk, kuanzia msimu ujao Samatta
atavaa jezi namba 10 ambayo awali ilikuwa ikivaliwa na kiungo
mshambuliaji Tino-Sven Susic raia wa Bosnia na Herzegovina.
Samatta
alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe na hadi sasa ameichezea mechi 51
na kufunga mabao 17 na amekuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu katika
kikosi cha timu hiyo.
Msimu
uliopita aliiwezesha Genk kufika robo fainali ya Europa League
wakitolewa na Celta de Vigo katika hatua hiyo kwa mabao 4-3 ambapo
katika mchezo wa kwanza ilifungwa 3-2 halafu ikatoka sare ya bao 1-1.
Bado Samatta ni mchezaji wa Genk, japokuwa zimekuwepo tetesi za mshambuliaji huyo kutakiwa na klabu nyingine.
0 comments:
Post a Comment