Na alanus
Mgombea
pekee wa nafasi ya ukatibu kwenye Chama cha Soka la Wanawake Tanzania
(TWFA), Somoe Ng’itu ameahidi kupambana kuhakikisha soka la wanawake
linapiga hatua ikiwa atachaguliwa kwenye nafasi hiyo.
Uchaguzi wa TWFA unatarajiwa kufanyika leo Jumamosi kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Chichi uliopo wilayani Kindondoni, Dar es Salaam.
Akizungumza
jijini Dar, Ng’itu alisema soka la wanawake limekua lakini bado
halijafikia kiwango kile kinachohitajika hivyo kama akipewa nafasi
atahakikisha anasaidia kuliinua yeye pamoja na wenzake watakaochaguliwa.
“Nikiwa
na mgombea wa nafasi ya ukatibu wa TWFA, ninaona soka la wanawake bado
halijafika katika kiwango kile kinachotakiwa hasa kupitia kwenye timu
yetu ya wanawake ya Twiga Stars.
“Hivyo,
basi katika kuhakikisha tunafikia katika ‘levo’ nzuri ile tunayohitaji
ni lazima niwepo kwenye uongozi wa TWFA na ndiyo maana nimeingia kwenye
kinyanganyiro hicho cha uchaguzi kwa kuwa ninaamini ninaweza kulikuza
soka letu kwa kushirikiana na wenzangu,” alisema Ng’itu.
Nafasi
zinazowaniwa katika uchaguzi huo ni uenyekiti, makamu mwenyekiti,
katibu, katibu msaidizi, mweka hazina, ujumbe wa mkutano mkuu wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na ujumbe wa kamati ya utendaji.
0 comments:
Post a Comment