Monday, June 11, 2018


Rafael Nadal amefanikiwa kutwaa taji la 11 la michuano ya French Open baada ya kumfunga Dominic Thiem raia wa Australia hatua ya fainali.

Mchezaji tennis huyo raia wa Hispania, Nadal ameshinda taji hilo la michuano ya wazi ya Ufaransa kwa kumfunga kijana mdogo, Dominic Thiem.

Mchezaji huyo anayeshika nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora duniania amechomoza na ushindi kwa jumla ya seti 6-4 6-3 6-2 na kuweka rekodi ya kutwaa mara 11.
Nadal ametwaa taji hilo mara 11 ambapo alianza kuchukua mwaka 2005,2006,2007,2008, 2010,2011,2012,2013,2014, kisha mwaka 2017 na mwaka huu 2018 akifanikiwa kulitetea taji lake.

0 comments:

Post a Comment