Kiungo wa kati wa
Lyon na Ufaransa Nabil Fekir, 24, alikuwa na matumaini makubwa kuwa
kuhama kwake kwenda Liverpool kungekamilika kiasi kwamba alikuwa tayari
amechagua namba ya shati lake. (L'Equipe, via Star)
Kipa wa Roma
Alisson, 25, yuko na furaha sana huko Roma licha ya Liverpool kummezea
mate kwa mujibu wa kocha wake Claudio Tafferel. (Tele Radio Stereo, via
Liverpool Echo)Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 28, atasalia klabu hiyo hadi meneja mpya ateuliwe licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kumsaini. (Independent)

Arsenal wanakaribia kumaliza kumsaini beki wa Freiburg na Uturuki Caglar Soyuncu , 22, baada ya ajenti wake kuthibitisha kuwa mazungumzo yamefanyika. (Turkish Football, via Sun)
Beki wa Barcelona Joel Lopez, 15, amefikia makubaliano na Arsenal. (Sport)

Real Madrid wanaandaa ofa ya pauni milioni 132 kumnunua kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic.
Mchezaji huyo wa miaka 23 pia anamezewa mate na Manchester United. (Il Messagero, kupitia Express)
Huenda Newcastle wasimwinde mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish ambaye thamani yake inawekwa kuwa pauni milioni 30. (Chronicle)

Newcastle inatathmini kumsaini mshambuliaji wa West Brom raia wa Venezuela Salomon Rondon, ambaye mkataba wake una kipengee cha pauni milioni 16. (Northern Echo)
Brighton, Crystal Palace, Southampton na West Brom wameonyesha nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Celtic Stuart Armstrong, 26, huku raia huyo wa Scotland akiwa na nia ya kuhamia Premier League. (Record)

Leeds wanaandaa ofa kwa mshambuliaji wa Derby na Jamhuri ya Czech Matej Vydra, 26, ambaye Derby wanataka kumuuza kuweza kupata fedha za kutumia. (Mail)

Bora kutoka Jumapili
Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah hajamsamehe nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos baada ya kuumizwa kulikomsababishia kuondoka uwanjani wakati wa fainali ya ligi ya mabingwa. (Marca, kupitia Mail on Sunday)Kiungo wa Dortmund na Ujerumani Mario Gotze 26 hawezi kuacha kufikiri uwezekano wa yeye kuungana na kocha wa liverpool Jurgen klopp ambaye aliwahi kuifundisha dortmund (DAZN, kupitia Independent)
Lyon wameachana na mpango wa kumuuza Nabil Fekir Kwa liverpool baada ya majogoo hao wa anifield kutaka kumpata kiungo huyo raia wa Ufaransa kwa bei pungufu ikiwa ni baada ya kufanyiwa vipimo vya Afya. (Sunday Mirror)
Liverpool ina mapango wa kumchukua mlinda mlango wa Burnley na England Nick Pope kwa pauni milioni 15.(Sun Jumapili)
Meneja wa Celtic Brendan Rodgers anatazamiwa na Leicester City kuwa huenda akamrithi Claude Puel. (Sun Jumapili)
Real Madrid imempatia mshambuliaji Cristiano Ronaldo mkataba wa thamani ya pauni milioni 28.5 kwa mwaka lakini huenda kisiwe kitita cha kutosha kwa mchezaji huyo . (Cadena COPE, kupitia Sunday Express)
Winga wa Stoke, Xherdan Shaqiri, 26, ameendelea kusita, bado hajafanya maamuzi ya kuhamia Liverpool. (Metro)
0 comments:
Post a Comment