Toure alifika mbali zaidi na kueleza kuwa ubaguzi unaofanywa na Pep Guardiola huwezi kuutambua kirahisi kwani ni mjanja sana, Toure alisema siku ikitokea kwenye kikosi cha Pep Guardiola akapanga first eleven yake wachezaji watano wa kiafrika, basi atanunua keki kumpelekea kama zawadi kitu ambacho anasema hakiwezi kutokea.
Baada ya tuhuma hizo kusambaa Pep Guardiola akiwa mapumziko kwao Hispania alihojiwa kuhusiana na tuhuma hizo na kujibu kwa kifupi tu “Toure anajua mimi sipo hivyo wewe unataka mimi nifanye nini nilikuwa pamoja na Toure kwa miaka miwili na alikuwa na siku 365 za kunieleza hisia zake, sio kitu muhimu kukizungumzia kwa sasa”>>> Pep Guardiola
0 comments:
Post a Comment