Monday, July 10, 2017



 Konta (kulia) hajawahi kushinda taji la Wimbledon

Andy Murray na Johanna Konta watapambana kuhakikisha kuwa wanafika robo fainali ya michuano ya Wimbledon ya wanaume na wanawake itakayochezwa siku ya leo.
Kama watafanikiwa itakuwa ndio kwa mara ya kwanza Uingereza kufanya hivyo tokea mwaka 1973.
Konta atapambana na Caroline Garcia katika mchezo wa ufunguzi.
Bingwa mtetezi Murray yeye atacheza na Benoit Paire siku hiyo ya Jumatatu.
Roger Federer, Novak Djokovic, Rafael Nadal na Murray kwa pamoja wameshinda vikombe 14 vya Wimbledon, huku mshindi mara tano Venus Williams akiwa ndiye pekee aliyeng'ara kwa upande wa kinadada.

0 comments:

Post a Comment