Kamati mpya ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tayari imekutana kwa mara
ya kwanza baada ya kuteuliwa mapema wiki iliyopita na Kamati ya Utendaji
ya TFF.
Mara baada ya kikao hicho cha
jana Jumamosi, Kamati imeweka hadharani majina ya wagombea wa nafasi
mbalimbali za uchaguzi, kinyang’anyiro kinachotarajia kufanyika Agosti
12, mwaka huu mkoani Dodoma.
Katika kinyang’anyiro hicho,
wagombea watatu wa nafasi ya urais hawakupitishwa akiwemo Jamal Malinzi
ambaye alikatwa kutokana na kutohudhuria usaili kinyume cha kanuni ya 11
(7) ya kanuni za uchaguzi za TFF.
Mgombea mwingine ambaye
hajapitishwa kuwania nafasi hiyo ni Fredrick Masolwa ambaye hajapitishwa
kwa kukosa uzoefu kwa mujibu wa kanuni ya 9 (3) ya kanuni za uchaguzi
za TFF.
John Kijumbe aliondolewa katika
kinyang’anyiro hicho kwa kukosa uzoefu huku Athumani Nyamlani alijitoa
kuwania uongozi wa Shirikisho hilo.
Waliopitishwa kuwania urais na
Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli ni Imani
Madega, Fredrick Mwakalebela, Wallace Karia, Ally Mayay, Shija Richard
na Emmanuel Kimbe.
Nafasi ya Makamu wa Rais
aliyejitoa ni Geofrey Nyange Kaburu ambaye anakabiliwa na tuhuma ya
makosa matano yakiwemo ya utakatishaji fedha kwa klabu ya Simba huku
waliopitishwa ni Mulamu Ng’ambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani,
Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.
Kwa mujibu wa Kuuli, zoezi
linalofuata kwa sasa ni kuhakiki kwa vyeti vya kidato cha nne kwa kila
mgombea baada ya kupitisha majina.
Kanda namba 1 ya Mikoa ya Kagera
na Geita: waliopitishwa ni Saloum Chama, Leopold Mukebezi na Kaliro
Samson huku Abdallah Mussa aliondolewa katika hatua za awali kwa
kutoambatanisha cheti cha elimu ya sekondari.
Kanda namba 2 inayounganisha
mikoa ya Mara na Mwanza: Vedastus Lufano, Ephraim Majinge, Samwel Daniel
na Aaron Nyanda (Wamepitishwa) huku Kanda namba 3 (Mikoa ya Shinyanga
na Simiyu) Stanslaus Nyongo, Mbasha Matutu na Bannista Rugora
(wamepitishwa).
Kanda namba 4 (Mikoa ya Arusha na
Manyara) waliopitishwa ni Omar Walii, Sarah Chao na Peter Temu
(wamepitishwa), Kanda namba tano inayounganisha mikoa ya Kigoma na
Tabora waliopitishwa ni John Kadutu, Issa Bukuku, Abubakar Zebo na
Francis Michael.
Kanda namba 6 yenye mikoa ya
Katavi na Rukwa Keneth Pesambili na Baraka Mazengo – wote wamepitishwa
huku Kanda namba 7 Mbeya na Iringa waliopitishwa ni Cyprian Kuyava,
Elias Mwanjala na Erick Ambakisye ilhali Abdusuphyan Sillah hajapitishwa
kwa kukosa uzoefu.
Kanda namba 8 mikoa ya Njombe na
Ruvuma waliopitishwa ni Golden Sanga, James Mhagama, Vicent Majili na
Yono Kevela huku Kanda namba 9 Lindi na Mtwara Athumani Kambi na Dunstan
Mkundi (wamepitishwa).
Kanda namba 10 Dodoma na Singida
waliopitishwa ni Hussein Mwamba, Steward Masima, Mohamed Aden, Ally Suru
na George Komba (wamepitishwa) huku Mussa Sima hajapitishwa kwa kukosa
uzoefu.
Kanda namba 11 Pwani na Morogoro
waliopitishwa ni Charles Mwakambaya, Gabriel Mkwawee na Francis Ndulane
huku Hassan Othuman hajapitishwa kwa kukosa uadilifu huku Kanda namba 12
Kilimanjaro na Tanga waliopitishwa ni Khalid Mohamed na Godluck Moshi
wamepitishwa wakati Thabity Kandoro hajapitishwa kwa kukosa uzoefu.
Kanda namba 13 Dar es Salaam:
waliopitishwa ni Abdul Sauko, Emmanuel Kazimoto, Ayoub Nyenzi, Shaffih
Dauda, Peter Mhinzi, Lameck Nyambaya, Mussa Kissoky, Said Tulliy, Ally
Kamtande, Aziz Khalfan, Ramadhani Nassib na Saad Kawemba.
Wakati Saleh Abdallah
hajapitishwa kwa kukosa uzoefu, Jamhuri Kihwelu na Bakari Malima
(hawajapitishwa kwa kushindwa kuwasilisha vyeti vya elimu ya sekondari)
0 comments:
Post a Comment