na alanus
Kaimu
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia
amewapa kongole viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake
(TWFA), waliochaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana kwenye
Ukumbi wa Hoteli ya Chichi, Dar es Salaam.
Katika uchaguzi huo uliopata
uwakilishi wa theluthi mbili ya mikoa yote ya Tanzania, Amina Karuma
alitetea kiti chake kwa kupata kura 47 kati ya 52 za wapigakura wote
huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikichukuliwa na Rose Kissiwa ambaye
aliyepata kura 42.
Mwanahabari Mkongwe wa Gazeti la
Nipashe kutoka Jumba la Magazeti la The Guardian, Somoe Ng’itu alishinda
nafasi ya Katibu Mkuu kwa kuvuna kura 49 ilihali Theresia Mung’ong’o
alishinda nafasi ya Katibu Msaidizi.
Hilda Masanche alishinda nafasi
ya Mweka Hazina wa TWFA kwa kupata kura 25 wakati Mwanahabari mwingine
Zenna Chande alishinda nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa
kupata kura 44.
Wajumbe Triphonia Temba, Mwamvita
Kiyogoma, Jasmine Soudy na Chichi Mwidege hawakushinda baada ya
wagombea wote wanne kutopata zaidi ya nusu ya kura kulingana na idadi ya
wapigakura kwa mujibu wa katiba ya TWFA.
Uchaguzi huo ulisimamiwa na
Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba,
ambaye pia aliwapongeza washindi.
Awali akifungua mkutano huo wa
uchaguzi, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Salum Madadi aliwataka wajumbe hao
kuwa makini katika kuchagua na kwamba si wakati wa kufanya mzaha katika
soka la wanawake.
0 comments:
Post a Comment