Friday, July 14, 2017


 Venus akisherekea ushindi

Matumaini ya Muingereza Johanna Konta kufika fainali za Wimbledon yamefutiliwa mbali baada ya kuchapwa na Venus Williams wa Marekani katika hatua ya nusu fainali.
Venus mwenye miaka 37 alicheza kwa umakini mkubwa zaidi na kushinda kwa seti 6-4 6-2.
Konta anayeshikilia nafasi ya sita kwa ubora duniani, alitegemea kufika fainali hizo na kuwa wa kwanza kufanya hivyo kwa Uingereza tokea mwaka 197

 Konta anasema alitegemea upinzani mkali kutoka kwa Venus
 Matumaini pekee kwa Konta ni kuingia ndani ya tano bora kwa ubora.
Venus atachuana na Garbine Muguruza wa Hispania aliyemchapa Magdalena Rybarikova wa Slovakia kwa seti 6-1 6-1.

0 comments:

Post a Comment