Ndege aina ya Air Bus A319-100 iliyokuwa imewabeba wachezaji wa Saudi Arabia imeshika moto nchini Urusi.
Ndege hiyo ilikuwa
imewabeba wachezaji wa Saudi Arabia ikisafiri kwenda katika mji wa
Rostov kwa ajili ya mechi yao ya pili dhidi ya Uruguay,
Katika mechi ya kwanza Saudi Arabia walifungwa mabao 5-0 na wenyeji Urusi na hadi sasa ndiyo timu iliyofungwa mabao mengi zaidi.
Hata hivyo, ndege hiyo
ilikuwa imekaribia kutua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Don,
bawa moja la kulia lilishika moto na kusababisha hofu.
Baadaye ilifanikiwa
kutua salama huku magari ya kuzima moto yakiwa yameizunguka na
kufanikiwa kuuzima moto huo huku wachezaji na viongozi wa Saudi Arabia
wakifanikiwa kushuka salama salimini.
0 comments:
Post a Comment